Thursday 28th March 2024
logo

TAARIFA MAALUMU.

TUME YA UTANGAZAJI ZANZIBAR

Tume ya Utangazaji Zanzibar inapenda kuwaarifu wale wote wanaomiliki leseni za Vituo vya Utangazaji vikiwemo Redio, Televisheni na Maudhui ya Mtandaoni kuwa, wanalazimika kufuata kikamilifu Muongozo wa Huduma za Utangazaji wakati wa Uchaguzi Zanzibar, 2020.
Muongozo huu utatumika kuwaongoza pamoja na Mawakala wa habari wanaofanya kazi Zanzibar wakati wa Uchaguzi Zanzibar.
Hata hivyo, Tume ya Utangazaji Zanzibar inasisitiza kwamba ipo macho na inafuatilia kwa ukaribu vyombo vyote vya utangazaji. Ni vyema vituo vya utangazaji vikafuata maelekezo ya Tume ya Utangazaji na Tume ya Uchaguzi katika kufanyakazi zao kwa uadilifu.
Kwenda kinyume na taratibu zilizowekwa hatua za kisheria zitachukuliwa.
Hivyo basi kila mmoja atawajibika kutoa taarifa kama ilivyoelekezwa ili kudumisha amani, mshikamano na utulivu katika nchi yetu.
Aidha napenda kutumia fursa hii kuwasisitiza wale wote wanaoendesha shughuli za utangazaji kupitia maudhui ya mtandaoni wakiwemo You tube na Bloggers, wafike Tume ya Utangazaji kujisajili,hii ni kutokana na kwamba Tume ya Utangazaji Zanzibar haitasita kuvichukulia hatua vyombo vyote vinavyoendesha huduma za utangazaji kinyume na kanuni ya Maudhui ya Mtandaoni ya 2020.
Ahsanteni.
Taarifa hii imetolewa na;
KATIBU MTENDAJI,
TUME YA UTANGAZAJI ZANZIBAR.
.

Other Top Story