Thursday 28th March 2024
logo

TUME YA UTANGAZAJI YAZINDUA MFUMO WA UFATILIAJI WA MAUDHUI YA MITANDAONI.

Katibu Mtendaji wa Tume ya utangazaji Zanzibar,Omar Said Ameir (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kuhusu mfumo wa ufatiliaji maudhui ya mtandaoni kwa katibu mkuu wizara ya habari utalii na mambo ya kale bi khadija bakari(wa kwanza kushoto) ambae alizindua rasmi mfumo huo

TUME ya Utangazaji Zanzibar imepongezwa kwa juhudi zake katika kusimamia vyema vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na kutafuta njia za kisasa ili kuhakikisha maadili ya Utangazaji yanafuatwa.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Khadija Bakari mara baada ya kuzindua mfumo wa Ufuatiliaji Maudhui ya Mtandaoni na Tovuti.

Amesema, Tume ya Utangazaji inafanya kazi nzuri hasa ikizingatiwa mfumo huo utaweza kufuatilia kwa karibu taarifa zinazoingizwa kupitia mitandaoni.
“Ninaipongeza Tume ya Utangazaji Zanzibar kwa kazi zake na hatua zinazochukuliwa katika kuendeleza na kudhibiti mawasiliano

Wakati huohuo, amewasisitiza waandishi wa habari kuitumia vyema tasnia ya habari kwa kujiepusha kutoa habari za uchochezi ambazo kwa namna moja ama nyengine zinaweza kuvuruga amani ya nchi iliyopo.
“Waandishi wa habari, nasisitiza mufanye kazi kwa uadilifu kwa kutoa taarifa sahihi na kuunganisha jamii ili kuepusha uchochezi unaoweza kuhatarisha utulivu na amani iliyopo,” alisisitiza.
Tume ya Utangazaji Zanzibar imeundwa kwa sheria nambari saba ya mwaka 1997 ambapo jukumu lake kuu ni kusajili na kutoa leseni za vyombo vya utangazaji, kudhibiti mawimbi ya sauti , vyombo vya utangazaji na kulinda utamaduni wa Mzanzibari.


.

Other Top Story